Andiko: Kumbukumbu la Torati 28:6: “Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.”
Ninaomba maisha yenu yajazwe upendo na baraka za Mungu. Sasa ningependa kushiriki nanyi neema kupitia ujumbe wenye kichwa “Mlango wa Baraka Umefunguliwa.” Huenda watoto wengi wa Mungu wamepokea baraka zake kuu na pia wameguswa kwa upole na Mungu, anayewajazia kila kitu wanachohitaji. Hivyo, huenda umeshangaa na kusema, “Hiki ndicho hasa nilichohitaji.”
Au huenda umeshukuru kwa upendo wa Mungu, aliyegusa mioyo ya wengine na kuwafanya wakupatie vitu ulivyohitaji. Hili hutokea kwa watoto wake watiifu. Mshiriki mmoja wa kanisa langu aliwahi kupanua biashara yake kupita kiasi, akitegemea uwezo wake mwenyewe, naye akaishia kuwa na deni la dola za Marekani 100,000. Tangu wakati huo alikabiliwa na shinikizo la wadai kadhaa, nyumba yake ikapigwa mnada, na familia yake, pamoja na watoto wadogo na mkewe, ikazurura huku na huku.
Alikuwa maskini sana kiasi kwamba mtoto wao mchanga hakuweza kupata maziwa. Wakati huo akatafakari maisha yake ya zamani, akatubia kwa dhati kutotii kwake kote Neno la Mungu na kuyaacha. Baada ya hapo aliweza kuwa na furaha moyoni hata alipokuwa akisafisha mifereji ya maji taka na mashimo ya maji taka. Haidhuru alipata kipato kidogo kiasi gani, kwanza alimtolea Mungu zaka kamili ya mapato hayo na kuendesha maisha yake kwa kilichobaki.
Alipoanza kulitii Neno la Mungu katika mambo hayo madogo, Mungu alimfungulia milango ya baraka na akawa mwakilishi wa kampuni iliyokuwa na wafanyakazi kadhaa. Baadaye akapata nafasi ya kupokea baraka kubwa zaidi. Alikumbuka Neno la Mungu lisemalo, “Usiisahau neema uliyopokea,” naye akaweka kiasi fulani cha fedha katika akaunti za benki za watu waliokuwa wamemsamehe baadhi ya madeni yake.
Angeweza kupuuza jambo hilo kwa sababu alikuwa amesamehewa madeni yake zamani, lakini alitii sauti ya Roho Mtakatifu aliyokuwa amesikia. Matokeo yake, mauzo yote ya kampuni yake yaliongezeka kwa asilimia 50 ndani ya mwezi mmoja tu, na sasa yanaendelea kuongezeka. Je, yeye peke yake ndiye aliyepokea baraka za Mungu? Mungu huwabariki hakika wote wanaojitahidi kulitii Neno lake na kuwa waaminifu kwa Ufalme wa Mungu.
Kumbukumbu la Torati 28:2 inasema, “Baraka hizi zote zitakujilia na kukupata ukiisikia sauti ya Bwana, Mungu wako,” na mstari wa 6 unasema, “Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.”
Kwa hiyo, Mungu anaahidi kuwabariki wale wanaolifuata Neno lake. Ninaomba kulitii Neno la Mungu na sauti ya Roho Mtakatifu, kupokea baraka kamili kupitia mlango wa baraka uliofunguliwa, na kumletea Mungu utukufu mkuu. Ninaomba haya katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo!
His Emeritus Bishop Dr. Jaerock Lee
Hii ina maana kwamba hata uovu mdogo ulio nao unaweza kukua na kuwa dhambi za wazi unapopata mazingira na hali zinazouwezesha.
Ninaomba maisha yenu yajazwe upendo na baraka za Mungu. Ningependa kushiriki nanyi neema kupitia ujumbe wenye kichwa “Mlango wa Baraka Umefunguliwa.”
Yonathani alikuwa mwana wa kwanza wa Sauli, mfalme wa kwanza wa Israeli. Ilitarajiwa kwamba angeketi kwenye kiti cha enzi baada ya Sauli, lakini Mungu alimtia mafuta Daudi awe mfalme wa Israeli.